Nitarejea

Album cover art for "Nitarejea" by Diamond Platnumz & Hawa Ntarejea

Diamond Platnumz & Hawa Ntarejea - Pop, Bongo Flava

Nitarejea

5.7K Plays

Duration: 3:34

Lyrics

Language:

[Intro: Diamond Platnumz] Ah ah ah... [Verse 1: Diamond Platnumz] Vipi mizigo umeshaweka tayari Mmmh, ah ah Sijechelewa nkaachwa na gari Mmmh, ah ah Basi jikaze usilie mpenzi Ah ah ah Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi Ah ah ah Zile taabu na njaa Msimu mzima mavuno hakuna Huwa nakosa raha Pale mkikosa cha kutafuna Roho yangu inauma Sema ntafanya nini Na pesa sina Nakuonea na huruma Bora niende mjini Kusaka tumaa [Chorus: Diamond Platnumz] Kama watoto wakinililia (kama) Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) Wadanganye na vibagia (wadanganye) Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama) Kama watoto wakinililia (kama) Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) Nawe usichoke kuvumilia (usichoke) Na kila siku kuniombea (nirude salama) [Verse 2: Hawa & Diamond Platnumz] Wanajua kwamba nafsi na roho Vitakuwa na wasiwasi... Ukumbuke na moyo Utajawa na simanzi... Ntakapokuwa nakwenda shambani Afu niko peke yangu honey Ntapokuja kuwa na majirani nitaumia Ah ah ah... Pale napotoka kisimani (ah ah) Ama nipo na kuni kichwani (ah ah) Sina wakunitua nyumbani nitalia Maneno yako yananfanya nakosa raha Na mawazo Hata mwenzako sijawahi kufika Dar Huu ndio mwanzo Vile nakwenda na sijui pa kukaa Wala mavasi, oh oh We niombee niepushwe na balaa Na maradhi, oh oh Eh eh [Chorus: Diamond Platnumz] Kama watoto wakinililia (kama) Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) Wadanganye na vibagia (wadanganye) Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama) Kama watoto wakinililia (kama) Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) Nawe usichoke kuvumilia (usichoke) Na kila siku kuniombea (nirude salama) [Bridge: Hawa & Diamond Platnumz] Unapokwenda kama ukifika salama Utukumbuke na sisi Usisahau kama mkeo na wana Umetuacha na dhiki Vile usijali ila naomba chunga sana Ogopa na marafiki Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama Waambie sidanganyiki Unapokwenda kama ukifika salama Utukumbuke na sisi Usisahau kama mkeo na wana Umetuacha na dhiki Vile usijali ila naomba chunga sana Ogopa na marafiki Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama Waambie sidanganyiki Eh eh [Interlude: Diamond Platnumz] Nitrarejea mama Niombee nirude salama Oh, watoto wadanganye Hii... Ooh ooh ooh, oh oh Tusale Usijali Hmm, kama... [Chorus: Diamond Platnumz] Kama watoto wakinililia (kama) Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) Wadanganye na vibagia (wadanganye) Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama) Kama watoto wakinililia (kama) Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama) Nawe usichoke kuvumilia (usichoke) Na kila siku kuniombea (nirude salama)

Rate this song

Rate this song

0/5.0 - 0 Ratings

5
0.0% (0)
4
0.0% (0)
3
0.0% (0)
2
0.0% (0)
1
0.0% (0)

Loading comments...

Credits

Writers
  • Hawa Ntarejea
  • Diamond Platnumz